Uchina
imesema imesikitishwa sana na mashtaka yaliyowasilishwa dhidi ya raia
wake sita na serikali ya Marekani kwa madai ya ujasusi wa kiuchumi.
Maafisa wa mashtaka wa Marekani wanadai kuwa wachina hao waliiba taarifa nyeti kutoka kwa kampuni za kiteknolojia zaMarekani zilizoko Silicon Valley ambako walikuwa wakifanya kazi ili kusaidia kampuni za Kichina kuwapiku kibiashara.
Washukiwa watatu kati yao ni Maprofesa.
Profesa Hao Zhang alitiwa mbaroni mjini Los Angeles lakini wengine watatu wako nchini Uchina.
Waandishi wa habari wanasema kuwa Uchina mara kwa mara hupuuzilia mbali madai ya ujasusi lakini inaonekana kuwa dhana hiyo inaendelea kukubalika nchini Marekani.
No comments
Post a Comment