Ujenzi wa bandari ya pili nchini Kenya katika Kaunti ya Lamu unatarajiwa kuzinduliwa rasmi wiki ijayo.
Mamlaka ya Bandari ya Lamu na Korido ya Usafiri ya Sudan Kusini na Ethiopia (LAPSSET) imethibitisha kuwa uzinduzi huo utafanyika Jumatatu wiki ijayo sambamba na Siku ya Afrika. Mkurugenzi LAPSSET Sylvester Kasuku amenukuliwa akisema kuwa Mei 25, Rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuongoza uzinduzi wa ujenzi wa bandari hiyo. Duru zinaarifu kuwa viongozi kadhaa wa eneo la mashariki mwa Afrika watahudhuria uzinduzi huo. Aidha anasema ofisi za bandari na kituo cha polisi ambazo ziko tayari, zitafunguliwa rasmi siku hiyo. Mamlaka ya Bandari ya Kenya inasema iko tayari kwa ujenzi wa bandari hiyo itakayogharimu mabilioni ya fedha. Bandari mpya ya Lamu inatazamiwa kuwa ya pili kwa ukubwa barani Afrika baada ya ile ya Durban Afrika Kusini. Serikali ya Kenya imeshaanza kutoa fidia kwa watu ambao ardhi zao zimechukuliwa ili bandari hiyo iweze kujengwa.
Mradi mzima wa LAPSSET unatazamiwa kugharimu Shilingi trioni 2.5 za Kenya au dola bilioni 25 za Kimarekani na utajumuisha ujenzi wa vituo vya kusafishia mafuta, reli, barabara, bomba la mafuta, viwanja vya ndege vitatu ikiwa ni pamoja na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Manda eneo la Lamu na ujenzi wa miji katika maeneo ya Lamu, Isiolo na Ziwa Turkana.

No comments
Post a Comment