Friday, 8 May 2015

DAVID CAMERON AELEKEA KUSHINDA UCHAGUZI MKUU UINGEREZA

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron anayewania kiti hicho. WAZIRI Mkuu wa Uingereza, David Cameron, anaelekea kupata ushindi mkubwa... thumbnail 1 summary

Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron anayewania kiti hicho.

WAZIRI Mkuu wa Uingereza, David Cameron, anaelekea kupata ushindi mkubwa katika uchaguzi mkuu uliofanyika jana nchini humo.
David Cameron katika pozi.
Matokeo ya awali mpaka sasa yanaonesha chama chake cha Conservative kimejiongezea hadi sasa jumla ya viti 20 na kupata ushindi katika majimbo 279 ambapo chama kikuu cha upinzani cha Labour kimepata jumla ya viti 217, hii ikiwa na viti 25 chini ya idadi iliyokuwa nayo katika bunge lililopita
Wakati matokeo ya theluthi moja ya majimbo yakiwa yametangazwa, Cameron anaonekana kurejea ikulu lakini bila idadi kubwa ya wabunge, jambo linalomaanisha chama cha Conservative kitalazimika kuunda serikali ya muungano.
Cameron amesema kuwa anapania kuendelea kuiongoza Uingereza ambayo iko chini ya muungano.
Shirika la habari la Uingereza ( BBC)  linakisia kuwa Cameron na chama chake huenda wakapata ushindi katika majimbo 329. GL mei 8 2015

No comments

Post a Comment