Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeahidi kurejesha
amani na usalama katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo yanayokabiliwa
na hali ya kuzorota usalama. Serikali ya nchi hiyo imesisitiza kuwa,
itachukua hatua za lazima kwa shabaha ya kurejesha usalama katika maeneo
ya mashariki mwa nchi hiyo. Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo imesema katika taarifa yake hiyo kwamba, haitaacha kuchukua hatua
yoyote ile itakayosaidia kurejesha amani na usalama katika maeneo hayo.
Taarifa ya serikali ya Kinshasa imekuja siku chache tu baada ya
kushuhudiwa mauaji mtawalia dhidi ya raia katika mkoa wa Beni ulioko
mashariki mwa nchi hiyo. Makumio ya watu wameuawa wiki iliyopita, hali
ambayo imezusha wasiwasi mkubwa miongoni mwa wakazi wa maeneo hayo.
Taarifa zaidi zinaonesha kuwa, waasi wa Uganda wa ADF-NALU ndio
wanaofanya mauaji hayo. Vikosi vya usalama vya serikali na vile vya
kusimamia amani vya Umoja wa Mataifa MONUSCO vinakosolewa kwa kushindwa
kulinda roho za raia katika maeneo hayo hasa mkoani Beni.
Tuesday, 19 May 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments
Post a Comment