Ban Ki moon, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa,
uvamizi wa Saudi Arabia nchini Yemen umeyatia nguvu makundi ya kigaidi
na kuyafanya yajizadidi na kushadidisha mashambulizi yao nchini Somalia.
Ban amenukuliwa na shirika la habari la Associated Press akisema hayo
jana katika ripoti yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na
kuongeza kuwa, usalama wa Somalia na eneo hilo zima la Pembe na Afrika
na mashariki mwa bara hilo unatishiwa na uwepo wa wanamgambo wa ash
Shabab wenye mfungamano na al Qaida. Matamshi hayo yamekuja katika hali
ambayo tarehe 9 mwezi huu wa Mei, makundi ya kitakfiri yalitangaza
kuhusika na mauaji ya Mbunge wa Puntland nchini Somalia, Said Hussein
Nur, siku moja baada ya mbunge huyo kupigwa risasi na kundi la watu
waliokuwa wamejizatiti kwa silaha wakati alipokuwa anatoka msikitini.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amehusisha matukio hayo na mashambulizi
ya Saudi Arabia nchini Yemen hususan kutokana na kuongezeka harakati za
kigaidi za makundi ya kitakfiri nchini Somalia tangu Saudia ilipoanzisha
mashambulizi dhidi ya wananchi wa Yemen. Nur ni mbunge wa pili wa
Puntland kuuawa katika kipindi cha wiki chache zilizopita. Mwezi
uliopita pia, wanamgambo wa ash Shabab walimuua kwa kumpifa risasi
mbunge mwengine Aden Haji Hussein wakati alipokuwa ziarani mjini
Mogadishu.
Tuesday, 19 May 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments
Post a Comment