Thursday, 14 May 2015

EAC yalaani mapinduzi nchini BURUNDI

Thu May 14 2015 Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika ... thumbnail 1 summary
Thu May 14 2015
Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
Wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamelaani vikali mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika nchini BURUNDI.

Akizungumza mara baada ya kikao cha wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya hiyo jijini DSM, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais JAKAYA KIKWETE amesema viongozi wanalaani mapinduzi hayo na ghasia nchini BURUNDI huku wakishauri uchaguzi mkuu nchini BURUNDI kuahirishwa.

Viongozi hao wanatarajia kukutana tena katika kipindi cha wiki mbili zijazo kujadili suala hilo.

Mkutano huo ulioitishwa kujadili hali ya BURUNDI na kujadili ripoti ya mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Afrika Mashariki waliokwenda nchini BURUNDI kutathmini hali ilivyo nchini hmo umehudhuriwa na Rais UHURU KENYATTA wa KENYA, Rais YOWERI MUSEVENI wa UGANDA, Rais PAUL KAGAME wa RWANDA, Makamu wa Rais wa AFRIKA KUSINI CYRIL RAMAPHOSA, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika NKOSAZANA DLAMINI ZUMA na mwakilishi kutoka nchini ANGOLA.
tbc

No comments

Post a Comment