Thursday, 14 May 2015

Milio ya risasi yasikika usiku Bujumbura

Kumekuwa na mapigano usiku kucha katika mji mkuu wa Burundi ambako kulikuwa na jaribio la mapinduzi ya kutaka kumng’oa m... thumbnail 1 summary

Kumekuwa na mapigano usiku kucha katika mji mkuu wa Burundi ambako kulikuwa na jaribio la mapinduzi ya kutaka kumng’oa madarakani rais, Pierre Nkurunziza.
Rais huyo ameshindwa kurejea nchini mwake kutoka katika mkutano wa viongozi wa kanda,baada ya ndege yake kugeuza kurejea ilikotokea.
Ingawa askari watiifu kwa rais huyo wamedai kuzima jaribio hilo la mapinduzi yaliyokuwa yakiongozwa na meja jenerali Godefroid Niyombare dhidi ya rais wao,na kwamba udhibiti wan chi uko mikononi mwao na hasa katika maeneo muhimu ya mji mkuu wan chi hiyo ,Bujumbura.
Makabiliano ya risasi yamesikika karibu na vituo vya redio na runinga .mwandishi wa BBC aliyeko nchini Burundi amesema kwamba ameshuhudia jeshi likiwa limegawanyika pande mbili ,na haijulikani nani ameshikilia udhibiti wa nchi kwa sasa.
Meja jenerali Godefroid Niyombare
Rais Nkurunziza amekosolewa kwa haja yake ya kuwania muhula wa tatu wa uongozi nchini Burundi ,maamuzi ambayo yalisababisha wiki kadhaa za maandamano ambapo watu ishirini wameripotiwa kupoteza maisha.

No comments

Post a Comment