Saturday, 23 May 2015

HAKUNA KUKWEPA JKT, WALIOKWEPA LAZIMA WASAKWE

Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa katika kikosi cha 824 KJ Kanembwa wakiwa tayari kwaajili ya Gwaride. PICHA YA MAK... thumbnail 1 summary
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiGihmk3veoP4A4GIs3n5DxfOBs0fju0VRfob2wGArQdVBZbKnDnp095gXXgf4UkeTXHoNUdoqohI8bk3m43OU_ruyrzv3bROD__37_gqbCPEH6FAWh4pwm-qxqI880-QQWDLinBlrULW8/s1600/MAFUNZO.JPG

Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya Jeshi la kujenga Taifa katika kikosi cha 824 KJ Kanembwa wakiwa tayari kwaajili ya Gwaride. PICHA YA MAKTABA.

WAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi amesema vijana wote waliohitimu kidato cha sita mwaka 2013/14, 2014/15 na kutojiunga na mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) bila ridhaa ya jeshi hilo, wanaendelea kusakwa na kuorodheshwa kwenye orodha ya watoro na upo uwezekano wa wao kwenda mafunzo hayo mapema mwezi ujao.


Akiwasilisha hotuba ya wizara hiyo bungeni jana ya Makadiro ya Mapato na Matumizi ya fedha kwa mwaka 2015/16, Dk Mwinyi alisema mafunzo ya JKT kwa wahitimu hao hutolewa kwa mujibu wa Sheria, ambapo ni ya kuwajengea uzalendo, ukakamavu, maadili mema, utaifa na kutoa stadi za kazi.

Alisema kwa mwaka 2014/15 jumla ya vijana waliopata mafunzo hayo kwa mujibu wa sheria ni 31,635 ambayo ni sawa na ongezeko la vijana 15,632, ukilinganisha na vijana 16,003 waliohitimu mafunzo hayo mwaka 2013/14 .
https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiOZfnfLkQJfenVttq0fXkATBkFJQXtRDMHHhau4hcEw4YbT6K9C07MhuiBg2v84Q_IAgyXo4qIwfiS5Yz7mwEEt-V1oOn6ymayqTvZvRycNAKSfimxvNxZ6IR7K2lW-5RMrVpcGadV_rU/s1600/unnamed+(74).jpgWAZIRI wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi.

 “Hata hivyo idadi hiyo ni pungufu ikilinganishwa na idadi ya vijana 41,000 waliohitimu kidato cha sita, waliostahili kujiunga na mafunzo hayo, na sababu zilizofanya upungufu huo ni pamoja na kalenda ya awamu ya pili ya mafunzo kugongana na kalenda ya kuanza mihula ya masomo ya elimu ya juu”, alisema Dk Mwinyi.

Na kuongeza vijana waliopaswa kujiunga na mafunzo hayo ila hawakujiunga bila ridhaa ya jeshi, wameingizwa kwenye orodha ya watoro wa jeshi hilo na kwamba wizara inaangalia uwezekano wa kuiwezesha JKT, kuchukua kundi hilo wakiwemo watoro, kuanza kwa mkupuo mmoja mafunzo hayo Juni hadi Agosti mwaka huu.

No comments

Post a Comment