Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, Iran kamwe haitoruhusu kukaguliwa vituo vyake vya kijeshi.
Ayatullahil Udhma Sayyid Ali Khamenei amesema hayo asubuhi ya leo (Jumatano) katika sherehe za kuhitimu masomo wanafunzi wa Chuo Kikuu cha maafisa wa kijeshi cha Imam Husain AS.
Aidha amegusia namna baadhi ya madola yalivyoingiza siasa za kupenda kwao makuu katika mazungumzo ya nyuklia ya Iran na kundi la 5+1 ikiwa ni pamoja na kutaka wavikague vituo vya kijeshi vya Iran pamoja na kuzungumza na wanasayansi wa nyuklia wa Iran na kusisitiza kuwa, ruhusa kama hiyo kamwe hawatapewa na maadui watambue kwamba, wananchi na viongozi wa Iran kwa vyovyote vile hawatolegeza misimamo yao katika kukabiliana na ubeberu na kupenda makuu madola hayo.
Ayatullahil Udhma Khamenei ametaja moja ya changamoto zinazoikabili Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kuwa ni ubeberu na kupenda makuu upande wa pili inaofanya nao mazungumzo ya nyuklia na kusisitiza kuwa: Hadi hivi sasa maadui hawajawatambua vizuri wananchi na viongozi wa Iran na ndio maana wanafanya ubeberu kama huo wakisahau kuwa wananchi na serikali ya Iran iliyotokana na wananchi hao, kamwe haitokubali kupigishwa magoti na ubeberu huo.
Amesema, kulegeza kamba kwa namna yoyote ile kutawafanya mabeberu hao watake makubwa zaidi na kusisitiza kuwa, inabidi taifa la Iran lijenge ukuta madhubuti utokanao na azma na nia ya kweli, kutawakali kwa Mwenyezi Mungu na kutumia vizuri nguvu zake za kitaifa katika kukabiliana na tabia ya kupenda makuu madola hayo.
Pia amesema kwa kusisitiza kuwa, viongozi wa Iran wanaoshiriki kwenye mazungumzo ya nyuklia wanapaswa kuonesha utukufu na nguvu za taifa la Iran katika mazungumzo hayo.

No comments
Post a Comment