Maafisa wa Israel wameahidi kupambana na ukatili wa polisi pamoja na ubaguzi dhidi ya Wayahudi kutoka Ethiopia.
Maandamano ya hivi karibuni yamezuka baada ya vidio kuonesha maafisa wawili wa polisi wakimshambulia mwanajeshi Muisrael mweusi akiwa katika sare za jeshi.
Kufuatia mkutano na viongozi wa kijamii, waziri mkuu Benjamin Netanyahu amesema ubaguzi katika jamii ya Israel ni tatizo kubwa ambalo linahitaji kushughulikiwa.
Ni katika mwaka 1984 ambapo Wayahudi kutoka Ethiopia waliruhusiwa kwa mara ya kwanza kuhamia nchini Israel chini ya sheria ya nchi hiyo ya kurejea ambayo inawaruhusu Wayahudi duniani kuwa raia wa Israel. source DW
No comments
Post a Comment