Kundi la Dola la Kiislamu limedai kuhusika na shambulio lake la kwanza nchini Marekani mjini Texas baada ya tukio nje ya ukumbi uliokuwa na mkusanyiko wa watu wanaopinga Uislamu mjini Texas siku ya Jumapili.
Maafisa wamefichua kuwa mmoja kati ya watu waliouwawa na polisi, alikuwa anachunguzwa kutokana na kuvutiwa na wapiganaji wa Jihadi.
Watu wawili wamefyatua risasi nje ya kituo cha makutano, mahali ambapo kulikuwa kunafanyika shindano la kumchora kwa dhihaka mtume Muhammad, shindano lililoandaliwa na vuguvugu la kulinda uhuru nchini Marekani.
Kwa mujibu wa dini ya Kiislamu, kumchora mtume Muhammad kunaonekana kuwa ni kufuru. Vyombo kadhaa vya habari nchini Marekani vimewatambua washambuliaji hao kuwa ni Elton Simpson mwenye umri wa miaka 31 na Nadir Soofi mwenye umri wa miaka 34, licha ya kuwa haijathibitishwa rasmi.
No comments
Post a Comment