Waitaka iainishe utaratibu utakao wawezesha kutumia haki yao ya kikatiba katika Uchaguzi Mkuu ujao
Dar es Salaam. Shirikisho la Wanafunzi Wanachadema wa Vyuo Vikuu (Chaso), limeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kueleza utaratibu wa kuwaandikisha wanafunzi katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili nao wapate fursa ya kushiriki Uchaguzi Mkuu ujao.
Dar es Salaam. Shirikisho la Wanafunzi Wanachadema wa Vyuo Vikuu (Chaso), limeitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kueleza utaratibu wa kuwaandikisha wanafunzi katika Daftari la Kudumu la Wapiga Kura ili nao wapate fursa ya kushiriki Uchaguzi Mkuu ujao.
Kaimu Mratibu wa Chaso, Dar es Salaam, Wilfred Mwalusanya alisema jana kuwa wanafunzi wengi walishindwa kupiga kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 kwa sababu walikuwa vyuoni.
Alidai kuwa wengi wao walipoteza haki yao ya msingi ya kuchagua viongozi wanaowataka kwa jambo ambalo tume ingeweza kuliwekea utaratibu maalumu wa kuwasaidia kupiga kura wakiwa vyuoni.
“Hatutaki hili lijirudie tena, tume itueleze imeandaa utaratibu gani wa kutuwezesha wanafunzi wa vyuo vikuu kushiriki Uchaguzi Mkuu, ” alisema Mwalusanya.
Aliongeza kuwa vyuo vitafungwa kati ya Juni na Julai, wakifika huko tayari kazi ya uandikishaji itakuwa imemalizika, hivyo watakosa fursa ya kuandikishwa.
“Serikali ya CCM ikishirikiana na Tume ya Uchaguzi tunahisi huenda wanafanya njama ili wanafunzi wa vyuo vikuu wasishiriki kwenye uchaguzi kwa sababu wana mwamko. “Mwaka huu hatukubali, lazima tupewe haki yetu ya kikatiba,” alisema kiongozi huyo.
Akifafanua kuhusu malalamiko hayo, Mwenyekiti wa NEC, Jaji Damian Lubuva alisema sheria inataka mtu kupiga kura sehemu alikojiandikisha.
Aliwataka wanafunzi wafanye mawasiliano mapema ili kujua ni wapi wanataka kupigia kura.
Jaji Lubuva alisema inawezekana pia kwa mwanafunzi aliyejiandikisha sehemu moja kuhamisha taarifa zake kwenye kituo anachotaka kupigia kura.
Alisisitiza kuwa kazi ya uandikishaji lazima ifanyike mapema kabla ya uchaguzi.
“Jambo kama hilo nilikutana nalo Njombe nikawaeleza mtu akiwahi anaweza kuhamisha taarifa zake kwenda kwenye kituo anachotaka kupigia kura. Sioni kama suala hili lina shida yoyote,” alisema Jaji Lubuva.
Wakati huo huo, Ofisa habari wa Chaso, Japhet Maganga alisema wamebaini nia ya Serikali kutaka kumwongezea muda wa uongozi Rais Jakaya Kikwete kwa kutumia Katiba Inayopendekezwa ili aendelee kuwapo madarakani.
mwananchi.
mwananchi.
No comments
Post a Comment