MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema), amesema hajaona mgombea ubunge mwenye uwezo wa kupambana naye kwenye uchaguzi mkuu mwaka huu.
Kutokana na hali hiyo, amewataka wananchi wa jimbo hilo wajiandikishe kwa wingi katika Daftari la Kudumu la Wapigakura ili waweze kukiondoa Chama Cha Mapinduzi (CCM) madarakani.
Lema aliyasema hayo juzi mjini hapa, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari.
“Hali ya usalama na kisiasa Arusha ni nzuri, CCM hawapo Arusha. Kwa hiyo sina wasiwasi, tutawashinda kwa kura nyingi kuliko tulivyowahi kuwashinda.
“Lengo langu siyo Lema kushinda hapa, bali
lengo ni Lema kuwezesha majimbo ya jirani kuongozwa na Chadema kwa sababu uwezo
wangu na nguvu zangu siyo za kupambana katika jimbo kama Arusha Mjini.
“Hili jimbo nitaendelea kuliongoza, hakuna mtu wa kunishinda, bado nitaendelea kuongoza kwa sababu sijapata wa kupambana naye kutoka CCM,” alisema Lema.
Akizungumzia Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Lema alisema wanatarajia kuwa na mkutano wa hadhara katika viwanja
vya Ngarenaro, mjini Arusha keshokutwa. mtanzania
No comments
Post a Comment