Waziri wa mambo ya nje wa Israel asiyekhofia kusema chochote Avigdor Lieberman amesema kwamba chama chake ya Yisrael Baitenu hakitojiunga...
11:17
Waziri wa mambo ya nje wa Israel asiyekhofia kusema chochote
Avigdor Lieberman amesema kwamba chama chake ya Yisrael Baitenu
hakitojiunga na serikali ya mseto inayoundwa na waziri mkuu Benjamin
Netanyahu. Taarifa hizo zimetangazwa na vyombo vya habari nchini
humo.Tangazo hilo la kushtukiza limekuja siku mbili kabla ya muda wa
mwisho uliowekwa kwa Netanyahu kuwasilisha serikali yake mpya
aliyotarajia itakuwa ya mrengo wa kulia ikijumuisha watu wanaozingatia
dini. Lieberman amenukuliwa katika tovuti ya gazeti la Haaretz akisema
wamefikia uamuzi wa pamoja wa kutojiunga na serikali hiyo ya mseto.Chama
cha Liberman chenye msimamo mkali kinachowapinga waarabu kilishinda
viti sita katika uchaguzi wa mwezi Machi na kilitarajiwa kujiunga na
chama cha Netanyahu cha Likud katika serikali inayoundwa na vyama
sita.Hata hivyo hatua ya Lieberman haitomzuia Netanyahu kuunda serikali
bali itaipunguzia serikali yake wingi wa viti bungeni, kwa kuambulia
viti 61 tu badala ya 67 ambavyo ingevipata katika bunge lenye viti 120.
No comments
Post a Comment