Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis Van Gaal amempokonya mshambuliaji wa kilabu hiyo Robin Van Persie haki za kupiga mkwaju...
12:59
Mkufunzi
wa kilabu ya Manchester United Louis Van Gaal amempokonya mshambuliaji
wa kilabu hiyo Robin Van Persie haki za kupiga mkwaju wa penalti baada
ya kukosa mkwaju kama huo katika mechi dhidi West Brom.
Alipoulizwa
iwapo Van Persie angeendelea kama mchezaji aliyeorodheshwa kupiga
penalti kwa niaba ya kilabu hiyo alijibu ''hapana,amefika mwisho
wake.Kila mara anarejelea makosa hayo hayo aliongezea''.
''Wayne Rooney pia amekosa mkwaju wa penalti na unapokosa mkwaju huo basi ujue utapiga foleni''.,aliongezea Ushindi wa West Brom ulikuwa matokeo mabaya kwa upande wa Manachester United kwa mara ya tatu mfululizo.
Van
Persie mwenye umri wa miaka 31 alikuwa na fursa ya kusawazisha kufuatia
bao la Chris Brunty kunako dakika ya 63 baada ya refa Anthony Taylor
kumpata na Saido Berahino na makosa ya kuunawa mpira katika eneo la
hatari.
No comments
Post a Comment