Rais wa Colombia Juan Manuel Santos anasema kuwa utawala wa nchi hiyo
haujui ni watu wangapi ambao hawajulikani waliko kufuatia maparomoko
makubwa ya ardhi ambayo yamewaua zaidi ya watu 50.
Waakazi wa mji
wa magharibi wa Salgar wanasema kuwa nyumba wanakoishi watu maskini
zilisombwa na matope pamoja na mawe kufuatia mvua kubwa iliyonyesha eneo
hilo.Makundi ya uokoaji yanatafuta kwenye vifusi kujaribu iwapo yatapata manusura.
Rais ameitaja hali hiyo kuwa janga la kitaifa na kusema kuwa atazijenga upya nyumba zilizoaharibiwa.
No comments
Post a Comment