Mawaziri wa Afrika Mashariki kutoka nchi tano za Jumuiya ya
Afrika Mashariki (EAC), walikutana jana mjini Arusha kaskazini mwa
Tanzania na kujadili hali ya uchaguzi nchini Burundi na mwisho wa
mkutano huo wametoa maazimio matatu. Miongoni mwa maazimio hayo ni
kuitaka Tume ya Uangalizi ya Uchaguzi wa Burundi kutoka nchi za EAC,
inayoongozwa na Jaji Joseph Warioba kuendelea na kazi hiyo nchini humo
mara moja. Aidha, imeazimiwa kuwa, Mwenyekiti wa Baraza la Mawaziri wa
EAC, Dk Harrison Mwakyembe na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya EAC, Dk Richard
Sezibera kutembelea Burundi mapema iwezekanavyo kwa lengo la kujionea
hali halisi katika nchi hiyo. Vilevile mkutano huo, umewapa jukumu
mawaziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki kutembelea kambi za wakimbizi
zilizopo Rwanda na Tanzania kwa lengo la kujionea hali halisi ya maisha
ya wakimbizi katika kambi zote zilizopo katika nchi hizo.
Tuesday, 19 May 2015
Mawaziri EAC watoa maazimio matatu kuhusu Burundi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments
Post a Comment