Kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) Mei 9 mwaka 2014. Lakini, rais wa Sudani Kusini na mpinzani wake, hawakusiriki katika mazungumzo ya amani, Addis Ababa, Ethiopia. |
Jeshi la Sudan Kusini limesema linafanikiwa kuchukua ngome
kadhaa za waasi. Msemaji wa jeshi Philip Aguer amesema mji wa Bentiu na
Leer inaelekea kuwa mikononi mwa wanajeshi wa serikali
Umoja wa Mataifa umeendelea kulalamikia kudorora kwa hali ya
usalama katika majimbo ya unity na Upper Nile wakati huu wafanyakazi wa
Mashirika ya kutoa misaada ya kibinadamu yakiondoka katika majimbo
ambayo vita vinaendelea.
Mazungumzo ya amani ya kupata suluhu nchini Sudan Kusini yameshindikana.
Hali ya Sudan Kusini imechukua mkondo mpya kwani kumezuka kikundi
kipya cha waasi wanaoongozwa na Meja jenerali maarufu aliyetoroka
kutoka jeshi la serikali.
Tayari Meja Jenerali huyo Johnson Olony, ametungua helikopta mbili za
kijeshi zilizotumwa kushambulia ngome yake mpya huko Malakal, mji mkuu
wa jimbo lenye utajiri wa mafuta la Upper Nile.
Siku moja baada ya serikali ya Sudan Kusini kutangaza kuwa vikosi
vyake vimeudhibiti mji wa Malakal, ulioko Kaskazini mwa mji mkuu Juba,
mambo yamebadilika, kwani mapigano makali yamezuka kati ya waasi wa
kundi jipya la waasi na majeshi ya Sudan Kusini katika Malakal, mji mkuu
wa jimbo la Upper Nile.
No comments
Post a Comment