André Ayew, mchezaji kutoka Ghana akiwa pia kiungo wa kati wa OM.
Kiungo huyo wa kati wa Olympique de Marseille, mwenye umri wa miaka 25, amekabidhiwa tuzo hilo, baada ya Vincent Enyeama, mchezaji kutoka Nigeria, ambaye alitunukiwa tuzo hilo mwaka 2014. André Ayew hatoichezea tena OM katika msimu ujao, baada ya mkataba wake na klabu hiyo kumalizika.
André Ayew anaongoza dhidi ya Max Gradel, mchezaji kutoka Cote d'Ivoire katika orodha ya wachezaji bora wa Afrika katika michuano ya Ligi kuu ya Ufaransa.
André Ayew ametunukiwa tuzo la Marc-Vivien Foé linalotolewa kila mwaka na RFI/France 24, baada ya Marouane Chamakh (mwaka 2009), Gervinho (mwaka 2010, mwaka 2011), Younès Belhanda (mwaka 2012), Pierre-Emerick Aubamyang (mwaka 2013) pamoja na Vincent Enyeama (mwaka 2014).
Akiwa na umri wa miaka 25, kiungo huyo wa kati anakuwa mchezaji wa kwanza wa Ghana na mchezaji wa kwanza wa Marseille kuchaguliwa mchezaji bora wa Afrika wa michuano ya Ligi kuu ya Ufaransa. André Ayew amepokea tuzo lake Jumatatu Mei 18 mwaka 2015 katika mji wa Issy-les-Moulineaux, kwenye makao makuu ya France Médias Monde (FMM).
André Ayew amechaguliwa na timu ya majaji ambao ni waandishi wahabari 65 na washauri kadhaa. André Ayew amepata pointi 221, akimshinda Max Gradel kutoka Cote d'Ivoire ambaye amepata pointi 186 na Aymen Abdennour kutoka Tunisia ambaye amepata pointi 89. Idrissa Gueye kutoka Senegal amepata pointi 23 na Jordan Ayew , mdogo wa André Ayew amepata pointi 17.
RFI, mei 18
No comments
Post a Comment