Waziri Kerry azuru Somalia
Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani John Kerry amefanya ziara ya kushitukiza nchini Somalia leo, maafisa wamesema, akiwa waziri wa kwanza wa mambo ya kigeni wa Marekani kuzuru nchi hiyo ya pembe ya Afrika iliyoharibiwa kwa vita.Waziri Kerry atakuwa mjini Mogadishu kwa saa chache, na hakupangiwa kutoka nje ya eneo linalolindwa la uwanja wa ndege ambako atakutana na rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud na waziri mkuu Omar Abdirashid Ali Sharmake.
Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani Marie Harf amesema katika taarifa kwamba waziri Kerry amewasili katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu, akiimarisha nia ya Marekani kuunga mkono kipindi kuelekea demokrasia ya amani nchini Somalia.
Katika mkutano wake na maafisa wa serikali kuu na serikali za mikoa , atajadili ushirikiano wa kiusalama na hatua zilizopigwa na Somalia kuelekea katika kutimiza mageuzi na maendeleo nchini humo
No comments
Post a Comment