Madereva wa treni wa Ujerumani wameanza mgomo wa siku tano, ukiwa mgomo mrefu zaidi katika kile kinachoendelea kuwa mzozo mkubwa na waendeshaji wa kampuni ya usafiri wa treni nchini humo.
Waendesha treni za abiria wameanza mgomo wao asubuhi ya leo wakijiunga na waendesha treni za mizigo ambao tayari wameanza mgomo wao jana Jumatatu.
Chama cha madereva wa treni GDL kimesema madereva hawatarejea kazini hadi Jumapili saa tatu asubuhi.
Kampuni ya usafiri wa treni nchini Ujerumani Deutsche Bahn, imesema theluthi moja ya treni zitaendelea kufanya kazi chini ya mpango wake wa usaidizi.
Chama cha madereva wa treni GDL kinataka ongezeko la asilimia 5 ya mishahara na muda mfupi wa kazi lakini suala muhimu ni madai ya majadiliano kwa wafanyakazi wengine ikiwa ni pamoja na makondakta ambao kwa kawaida wanawakilishwa na chama tofauti cha wafanyakazi.
No comments
Post a Comment