Mashindano
ya taifa ya masumbwi nchini Tanzania huenda yakasogezwa mbele mpaka
mwezi July.Kuahirishwa huko Kunatokana na ombi la mkoa wa Kigoma kuomba
yasogezwe kutokana na maandalizi kutokamilika.
Mashindano hayo yalipangwa kufanyika mwezi Mei na yatatumika kuchagua mabonda kwa michuano mbalimbali ya kimataifa.Katibu mkuu wa Shirikisho la ngumi BFT, Makore Mashaga amenukuliwa akisema kuwa watakutana ili kujadili ombi hilo kabla ya kuchukua uamuzi wa kuyasogeza mbele au la.
Mashaga pia amesema maandalizi ya timu ngumi kwa ajili ya kujiandaa na michezo ya Afrika yanaendelea vizuri.
Michezo ya Afrika itafanyika nchini Congo Brazzaville mwezi Septemba mwaka huu huku zaidi ya wanamichezo 2,000 wakishiriki katika michezo tofauti.
No comments
Post a Comment