Friday, 8 May 2015

Membe amkabidhi Nkurunziza Rais wa Burundi maswali manne

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza aliyekaa mbele akizungumza na ujumbe ulioongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikia... thumbnail 1 summary

Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza aliyekaa mbele akizungumza na ujumbe ulioongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe alipokutana nao mjini Bujumbura nchini humo juzi. Na Mpigapicha Maalumu  Kikao hicho kinatarajiwa kufanyika Dar es Salaam, Mei 13, mwaka huu na kuhudhuriwa na marais wa jumuiya hiyo, kitajadili hali ya kisiasa Burundi.
Bujumbura. Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe juzi alikutana na Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza na kumwachia maswali manne atakayoyajibu katika kikao cha dharura cha Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kilichoitishwa na Rais Jakaya Kikwete ili kuokoa hali ya machafuko yanayohofiwa kutokea Burundi.

Kikao hicho kinatarajiwa kufanyika Dar es Salaam, Mei 13, mwaka huu na kuhudhuriwa na marais wa jumuiya hiyo, kitajadili hali ya kisiasa Burundi.

Hofu ya machafuko imejitokeza baada ya Rais Nkurunziza kutaka kugombea tena katika uchaguzi ujao, jambo linalopingwa na vyama vya upinzani na wanaharakati nchini humo.

Juzi, Waziri Membe aliwaongoza mawaziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Balozi Amina Mohammed na Rwanda, Louise Mushikiwabo kuzungumza na Rais Nkurunziza ili kujua ni jinsi ya kutatua mgogoro huo.

Maswali hayo ni kuhusu uchaguzi ujao kama utakuwa wa haki, amani, huru na endapo nchi itatawalika baada ya uchaguzi huo.

“Hatupendi vurugu na ndiyo maana tunataka kukutana kutatua tatizo lililopo,” alisema.

Tangu chama tawala cha nchi hiyo CNDD-FDD kimpitishe Rais Nkurunziza kuwania nafasi hiyo, maandamano ya kupinga uteuzi wake yalianza jijini Bujumbura.

Hivi sasa mitaa ya Bujumbura iko kimya, huku shughuli zote za kibiashara zikiwa zimesitishwa kutokana na polisi kuzuia mikusanyiko ya watu.

No comments

Post a Comment