Friday, 22 May 2015

Merkel asema EU hainuii kuibana Urusi

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya na nchi za Ulaya Mashariki ambazo awali zilikuwa sehemu ya Umo... thumbnail 1 summary
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema ushirikiano kati ya Umoja wa Ulaya na nchi za Ulaya Mashariki ambazo awali zilikuwa sehemu ya Umoja wa Kisovieti, sio mpango wa sera ya kuupanua Umoja wa Ulaya.
Bi Angela Merkel, Kansela wa Ujerumani Bi Angela Merkel, Kansela wa Ujerumani
Katika hotuba yake kwenye bunge la Ujerumani mjini Berlin leo kabla ya mkutano wa Umoja wa Ulaya na nchi hizo za Ulaya Mashariki, Bi Merkel amesema Ulaya haipaswi kuweka matumaini ya uongo ambayo haiwezi kuyatekeleza.
Hotuba hiyo ya Kansela Angela Merkel imetolewa muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano kati ya Umoja wa Ulaya wenye nchi 28 wanachama, na nchi sita za Ulaya ya Mashariki ambazo zilikuwa katika Umoja wa Jamhuri za Kisovieti, ambazo ni Ukraine, Belarus, Georgia, Armenia, Azerbaijan na Moldova. Mkutano huo unaanza leo katika mji mkuu wa Latvia, Riga.
Katika hotuba yake bungeni Bi Merkel amezungumza kuhusu mkutano wa kundi la nchi 7 zilizoendelea zaidi kiviwanda au G-7, ambalo kabla ya kupanuka kwa mzozo wa kisiasa na kivita nchini Ukraine lilikuwa likijumuisha Urusi. DW

No comments

Post a Comment