Maandamano ya waliyoyaitaya amani yaliyofanyika
Chuo Kikuu cha Dodoma asubuhi ya leo yamesambaratishwa na jeshi la polisi baada
ya kupata amri ya mkuu wao wa kikosi. Katika eneo la tukio maeneo ya katikati
ya Utawala mkuu na kitivo cha Elimu (COED) ndipo hali ya hatari ilipoanzia na
wanachuo wakaanza kusambaratishwa kutoka barabarani na mabomu ya machozi huuku
wakiamriwa kukaa na kutulia mabwenini kwao.
Mgomo huu umekuja baada ya nachuo kufanya maamuzi
hayo kuishinikiza serikali ya Jamhuri ya Muungano kuingfilia kati baadhi ya
masuala ambayo inaonekana utawala wa chuo unashindwa kutoa majibu sahihi naya kuridhisha.
Minongoni mwa hoja za wanafunzi ni kupinga ulipaji wa Bima ya afya mara mbili, na hata kutokupatiwa kadi za Bima hizo, pesa za kujikimu yaani BOOM, tatizo la wanachuo wanaoishi nje ya chuo kulipia vyumba chuoni, na ubadhilifu anaodaiwa kufanywa na serikali ya wanafunzi huku wakimuomba Waziri mkuu wa Nchi, mh. Mizengo Pin kuja kutoa tamko juu ya yote hayo. Hali bado ni shwari mapaka sasa ila bado haijafahamika wazi kuwa watarudi barabarani au la.
tembelea tegemeo la wote upate kuhabarika zaidi.
No comments
Post a Comment