Wednesday, 6 May 2015

MGOMBEA URAIS CHADEMA ATAPATIKANA JUNI 20

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza tarehe za wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kuchukua na kurejesha fomu, ambap... thumbnail 1 summary
Mchakato wa urais Chadema kuanza Julai 20CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza tarehe za wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kuchukua na kurejesha fomu, ambapo kwa nafasi ya Rais, zitatolewa Julai 20 na kurejeshwa Julai 25.
Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe alisema jijini Dar es Salaam jana, tarehe hiyo na za madiwani na wabunge kuchukua fomu, zimepitishwa na Kamati Kuu ya CHADEMA kwenye mkutano uliofanyika kwa siku mbili.
Kwa mujibu wa Mbowe, wabunge wataruhusiwa kuanza kuchukua fomu za kugombea nafasi hiyo kwa vipindi viwili tofauti, ambapo Mei 18 itakuwa siku ya watakaotaka kugombea Ubunge kwenye majimbo, ambayo kwa sasa chama hicho hakina wagombea.
Aidha, ilielezwa kuwa siku hiyo wanaowania nafasi ya Ubunge wa Viti Maalum nao wataruhusiwa kuchukua fomu na kuzirejesha na wanaowania Ubunge kwenye majimbo yasiyo na wabunge wa CHADEMA ifikapo Juni 25.
“Julai 6 itakuwa ni siku ya kuchukua fomu za ubunge katika majimbo ambayo chama chetu kina wabunge na Julai 10 ndio zitatakiwa kurejeshwa”, Mbowe alisema na kuongeza kuwa, Mei 18 itakuwa siku ya kuchukua fomu za Udiwani kwenye Kata ambazo chama chake hakina Madiwani, zitakazotakiwa kurejeshwa Juni 25.
Kwa upande wa kata ambazo kuna madiwani wa chama hicho, imeelezwa kuwa, fomu za Udiwani zitaanza kutolewa Julai mosi na kurejeshwa Julai 10, kuruhusu uteuzi wa mwisho wa wagombea Udiwani na wale wa Viti Maalum

No comments

Post a Comment