Wednesday, 6 May 2015

UWT Arusha wawakataa walimu uchaguzi mkuu

JUMUIYA ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Arusha, imetangaza wazi kuwakataa walimu kusimamia uchaguzi wa madiwani, wabunge ... thumbnail 1 summary
Wanawake wa UWT wakishangilia.
    JUMUIYA ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi (UWT) Mkoa wa Arusha, imetangaza wazi kuwakataa walimu kusimamia uchaguzi wa madiwani, wabunge na rais, kutokana na tabia ya kufanya hujuma kwa chama hicho wakati wanasaidiwa mambo mengi ya msingi na serikali ya CCM. Mbali ya walimu, pia UWT imewanyooshea kidole baadhi ya polisi mkoani Arusha kwa kuwa na mapenzi yaliyopitiliza dhidi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), hali inayowafanya kushindwa kutenda haki katika maamuzi mbalimbali. Msimamo huo umetangazwa kwa nyakati tofauti na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo mkoa wa Arusha, Flora Zelote alipokuwa akizungumza katika kata mbalimbali za wilaya ya Arusha katika ziara yake ya kikazi ya kukagua uhai wa jumuiya hiyo na chama kwa ujumla

No comments

Post a Comment