Thursday, 7 May 2015

mgomo wa mabasi utabaki historia

MGOMO wa madereva wa mabasi yaendayo mikoani, daladala na malori huenda usitokee tena nchini na hivyo kubaki kuwa suala la kihistoria. H... thumbnail 1 summary
Mgomo wa mabasi wasitishwa

MGOMO wa madereva wa mabasi yaendayo mikoani, daladala na malori huenda usitokee tena nchini na hivyo kubaki kuwa suala la kihistoria.
Hali hiyo inatokana na Serikali na viongozi wa madereva hao kukubaliana rasmi kumaliza migomo hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda ambaye juzi alijitwisha mzigo wa kuwa msuluhishi wa mgomo wa madereva kote nchini, alisema jana Dar es Salaam kuwa hawatakuwa na mgomo na kwamba hawategemei kuwa na mgomo wa aina hii tena nchini.
Makonda alisema kupitia malalamiko ya muda mrefu kutoka Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (Taboa) na Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (Tatoa), yatakuwa yakishughulikiwa katika Kamati iliyoundwa juzi.
Alisema kupitia Kamati hiyo ambayo inahusisha viongozi mbalimbali wa Serikali, watahakikisha kila dereva anapata mkataba kwani viongozi hao pia wanatamani madereva wapewe mikataba yao ili kuepukana na adha iliyotokea.
Makonda alisema pamoja na mambo mengine, wataunda mfumo rasmi wa kutambua ajira za madereva hao.
‘’Natangaza rasmi kwamba, mgomo wa madereva wote nchini hautakuwepo na kwamba hatutegemei kutokea tena nchini,’’ alisema Makonda.

No comments

Post a Comment