Idara ya AMD imeilaza mabo 3 kwa 1 idara ya DS Chuo
kiku cha Dodoma na kutamba kutinga fainali itakayochezwa saa kumi jioni ya
ijumaa tarehe 8 wiki hii. Idara ya AMD inaundwa na kozi za wasanii,
wanamitindo, wanahabari, pamoja na walimu kwa asilimia kubwa. Mashabiki wa Ds
waliwabeza walimu kwa kejeli kubwa huku wakisema, “ualimu ni stress, michezo
hamuwezi” huku wanaidara ya AMD wakiendelea kuishabikia timu yao vilivyo na
kuwapa nguvu wachezaji wake. AMD sasa inakabiliwa na kibarua kizito cha kumng’oa
meno bila ganzi PSPA au wao kunyolewa bila maji siku ya kesho ili waweze
kujitwalia zawadi ya ng’ombe mzima.
Zione picha za mashabiki wakiingia
uwanjani na wakiwa uwanjani.
No comments
Post a Comment