Diwani wa Soko la Tazara
Vetenary Zahoro Maganga akitoa maelezo kwa Mbunge wa Jimbo la Temeke
Abbas Mtemvu alipotembelea maeneo yaliyoharibiwa na mvua akiongozana
na viongozi wa Wakala wa Serikali wa Barabara (Tanroads) jinsi maji
yanavyotakiwa kufata mfereji huo ambao haupitishi maji kupeleka katika
mfereji huo (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Mbunge wa Jimbo la Temeke
Abbas Mtemvu (kulia) akizungumza na viongozi wa Wakala wa Serikali wa
Barabara (Tanroads) katika ziara ya kutembelea maeneo yaliyo haribiwa
na mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam (kushoto)
ni Meneja wa Tanroads Mkoa wa Dar es Salaam, Mhandisi Julius Ndyamukama.
Mhandisi Mradi Tanroads
Mkoa wa Dar es Salaam Ngusa Julius (wa pili kulia) akimwelekeza jambo
Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (aliye vaa kofia) wakati wa ziara
ya kutembelea maeneo mbalimbali ya jimbo lake yaliyo haribiwa na mvua
na kusaidia kutowa Mashine ya kuondoa maji hayo yaweze kuondolewa
(kushoto) ni Katibu wa Kamati ya maafa na miundombinu ya Soko la
Vetenary Manispaa ya Temeke Morocco Milanzi na kulia ni Naibu Meya
Manispa Temeke Juma Mkenga.
Katibu wa Kamati ya maafa
na miundombinu ya Soko la Vetenary Manispaa ya Temeke Morocco Milanzi
(wapili kulia) akizungumza na viongozi wa Wakala wa Serikali wa Barabara
(Tanroads) wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Temeke Abbas Mtemvu (wa
pili kushoto), wakati wa ziara ya kutembelea maeneo yaliyo haribiwa na
mvua zilizokuwa zikiendelea kunyesha Jijini Dar es Salaam na mbunge huyo
kusaidia mashine ya kuyaondosha maji hayo.
Baadhi ya maeneo waliyo kumbwa na maji katika Soko la Vetenary Manispaa ya Temeke.
Meneja wa Tanroads Mkoa wa
Dar es Salaam, Mhandisi Julius Ndyamukama akiwa na (wa tatu)kulia
akizungumza jambo wakati wa ziara na Mbunge Abbas Mtemvu wakati wa ziara
hiyo.
Mwenyekiti wa Serikali ya
Mta wa Kilimahewa Tandika Devis Coner Mfaume Mbonde (kulia) akielekeza
jambo wakati wa ziara ya Mbunge na viongozi wa Tanroads wakiangalia
maeneo yaliyoharibiwa na mvua nakuahidi kufanyia marekebisho maeneo
hayo.
source; mo blog
source; mo blog
No comments
Post a Comment