Karibu
magari milioni thelathini na nne yanarejeshwa viwandani nchini Marekani
ambako mifuko ya hewa ya usalama katika magari imelalamikiwa
kusababisha vifo vya watu wapatao watano.
Tukio hili la
urejeshwaji wa magari viwandani kutokana na kasoro za kiufundi ni kubwa
zaidi kuwahi kutokea nchini Marekani. Kampuni ya kutengeneza vifaa vya
magari ya Japan, Takata, imekiri mifuko ya hewa kulinda usalama wa
watumiaji wa magari kuwa na kasoro. Baadhi ya mifuko hiyo ya hewa
imepasuka kwa nguvu kupita kiasi na kusababisha kurusha vipande vya
chuma kwa madereva na abiria wanaokaa viti vya mbele. Waziri wa
Usafirishaji wa Marekani, Anthony Foxx, ametangaza kurejeshwa kwa magari
yenye hitilafu ya mfumo huo kote nchini humo.Bwana Foxx amesema urejeshwaji wa magari hayo ni kazi kubwa.
Tangazo hilo limetolewa na Utawala wa Usalama wa Taifa nchini Marekani katika Barabara Kuu baada ya mazungumzo marefu na kampuni ya Takata. Magari yanayorejeshwa yanahusu kampuni kumi na moja za kutengeneza magari zikiwemo za Honda, Toyota na Nissan.
Urejeshwaji viwandani kwa magari mapya hufanyika baada ya kugundulika hitilafu lolote la kiufundi linaloweza kuhatarisha usalama wa watumiaji wa magari
No comments
Post a Comment