Wednesday, 6 May 2015

MUSEVENI asema changamoto za afrika kutatuliwa na waafrika wenyewe

   Wed May 06 2015 Rais Yoweri Museveni wa Uganda Rais Yoweri Museveni wa Uganda amezungumza katika mjadala wa ngazi ya juu ku... thumbnail 1 summary
   Wed May 06 2015
Rais Yoweri Museveni wa Uganda
Rais Yoweri Museveni wa Uganda amezungumza katika mjadala wa ngazi ya juu kuhusu ushirikiano baina ya Umoja wa Mataifa na Mashirika ya kikanda uliofanyika kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini NEW YORK na kusema kuwa changamoto za AFRIKA zitatuliwe na viongozi wa AFRIKA.

Rais MUSEVENI amesisitiza umuhimu wa kusikiliza sauti za mashirika ya kikanda katika masuala ya amani ya kimataifa, huku akiongeza kwamba ni lazima kubadilisha mfumo wa Umoja wa Mataifa hasa Baraza la Usalama.

Amesema kuwa jamii ya kimataifa ikiwemo Umoja wa Mataifa inapaswa kuheshimu utaratibu wa kikanda.

Amesema utaratibu huo utasaidia kuzuia Umoja wa Mataifa kutumiwa kwa faida za kitaifa au vikundi vya wanachama wenye nguvu na kudhoofisha juhudi za mashirika ya kikanda na amani duniani.

Katika kikao hicho cha ngazi ya juu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amezingatia umuhimu wa mashirika ya kimataifa katika kukuza maendeleo endelevu na amani ya kimataifa kwenye kanda zao na haja ya kuimarisha uhusiano kati yao na Umoja wa Mataifa.

No comments

Post a Comment