Sunday, 3 May 2015

Muungano wa Saudi Arabia wakanusha kufanya mashambulizi ya Ardhini Yemen

Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia unaopambana na waasi wa Houthi nchini Yemen kupitia kampeni yake ya mashambulizi ya angani, umekanush... thumbnail 1 summary

Muungano unaoongozwa na Saudi Arabia unaopambana na waasi wa Houthi nchini Yemen kupitia kampeni yake ya mashambulizi ya angani, umekanusha madai ya vikosi vyake kuingia nchini Yemen, kufuatia ripoti kuwa vikosi hivyo vimeingia mjini Aden hii leo. Msemaji wa muungano huo brigadia Jenerali  Ahmed Assiri amelihakikishia shirika la habari la Al-Ekhbariya la Saudi Arabia kuwa hakuna vikosi vyoyvyote vilivyoingia Aden kupambana na waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran. Hata hivyo amesema kwa sasa hawezi kusema chochote juu ya mustakbal wa muungano huo au operesheni zinazoendelea lakini akasema hatua zote zinaweza kuchukuliwa.

No comments

Post a Comment