Sunday, 3 May 2015
Rais Faure Gnassingbe wa Togo ashinda kipindi kingine madarakani
Mahakama ya kikatiba nchini Togo imethibitisha Faure Gnassingbe
ameshinda muhula wa tatu kama rais kwa asilimia 58.77 ya kura, katika
uchaguzi uliofanyika tarehe 25 mwezi wa Aprili, na kumshinda mpinzani
wake ambaye ni kiongozi wa upinzani Jean-Pierre Fabre. Ushindi huo
katika uchaguzi uliofanyika kwa amani unaweza kurefusha muda wa familia
ya Gnassingbe kushikilia madaraka kwa zaidi ya nusu karne. Gnassingbe
amekuwa rais wa Togo kuanzia mwaka wa 2005 wakati babake alipofariki
baada ya kuwa madarakani kwa miaka 38 katika taifa hilo la Afrika
Magharibi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments
Post a Comment