Bariadi. Polisi mkoani Simiyu inamshikilia mkazi wa Kijiji cha Bukigi, Kata ya Malampaka wilayani Maswa, kwa tuhuma za kukutwa na viungo vinavyosadikiwa kuwa ni vya binadamu likiwamo fuvu la kichwa.
Mtuhumiwa huyo ambaye pia ni mwenyekiti wa kijiji
hicho na mganga wa kienyeji, alikamatwa nyumbani kwake baada ya kuwapo
kwa taarifa kuwa alikuwa amewahifadhi majambazi ili awazindike.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Simiyu, Gemini Mushi
alisema jana kuwa mwenyekiti huyo alikamatwa Mei 9, kijijini hapo baada
ya kupata taarifa ya kuwapo majambazi nyumbani kwa mwenyekiti huyo.
Alisema baada ya taarifa hizo, polisi walifanya msako nyumbani kwa
mwenyekiti huyo na kufanikiwa kukamata vitu hivyo.
Alisema polisi wanaendelea na uchunguzi ili
kubaini kama viungo hivyo ni vya binadamu na kama anahusika navyo, kwa
sababu vilikutwa nje ya nyumba yake.
mwananchi mei 14
mwananchi mei 14
No comments
Post a Comment