Wednesday, 6 May 2015

Ni vita ya Barcelona na Bayern Munich

6 Mei 2015 Mshirikishe mwenzako Timu ya Bayern Munich Kocha Pep Guardiola anarejea N... thumbnail 1 summary

6 Mei 2015

Timu ya Bayern Munich
Kocha Pep Guardiola anarejea Nou Camp kuiongoza Bayern Munich dhidi ya timu yake ya zamani Barcelona kwenye Nusu Fainali ya Klabu Bingwa barani Ulaya.
Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa ni mwaka 2013, katika mchezo wa Nusu Fainali ya Mashindano haya, Bayern Munich, waliwachapa Barcelona Jumla ya Bao 7-0 katika Mechi mbili.
Barcelona wameifunga Bayern Munich mara 1 tu katika Mechi 8 zilizopita za Ulaya na kutoka sare 2 na kufungwa 5.
Mechi hii inakutanisha makocha,waliokuwa wachezaji wa zamani wa Barcelona Luis Enrique wa Barcelona na Pep Guardiola kwa upande Bayern Munich.
Mchezo huu utachezwa kwenye dimba la Nou Camp, huko Hispania.

No comments

Post a Comment