Baadhi ya makamanda waliohusika na jaribio la mapinduzi ya kijeshi
lililofeli nchini Burundi, walipandishwa kizimbani katika mahakama ya
Bujumbura jana Jumamosi. Miongoni mwa watuhumiwa hao 17 ambao walitakiwa
kujibu mashitaka dhidi yao mbele ya mahakama, ni pamoja na Jenerali
Cyrille Ndayirukiye na viongozi wawili wa polisi. Hata hivyo Meja
Jenerali Godefroid Niyombare aliyeongoza jaribio hilo la mapinduzi bado
hajulikani alipo. Watuhumiwa hao walitiwa mbaroni jijini Bujumbura na
askari watiifu kwa Rais Pierre Nkurunziza baada ya rais huyo kurudi
Ikulu Ijumaa ya juzi ya tarehe 15 Mei. Kwa mujibu wa habari za hivi
karibuni, hali ya usalama mjini Bujumbura bado si shwari. Hii ni katika
hali ambayo wanaharakati wa haki za binaadamu, wameituhumu serikali ya
Rais Pierre Nkurunziza, kwa kukandamiza vyombo binafsi vya habari na
kutoa vitisho dhidi ya viongozi wa kisiasa wa upinzani. Serikali ya
Burundi inavituhumu vyombo hivyo vya habari kuwa vinawachochea wananchi
kumiminika mabarabarani jijini Bujumbura na kufanya maandamano ambayo
hadi sasa yameshapelekea kuawa watu wasiopungua 25
Sunday, 17 May 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments
Post a Comment