Kiongozi
wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis amewatawaza watawa wawili wa
Kipalestina walioishi katika karne ya 19 wakati wa utawala wa Ottoman
kuwa watakatifu.
Watawa hao wawili walioishi miongoni mwa jamii ya
wapalestina waarabu ,bi Marie Alphonsine Ghattas na Mariam Bawardy
watakuwa miongoni mwa watakatifu watakao tawazwa hii leo katika ukumbi
wa kanisa kubwa la papa Francis la St Peter's Square iliyoko Rome.Hatua hii inatazamwa na wengi kama chambo cha kuwavutia wakristu katika maeneo ya mashariki ya kati ambapo wakristu wanahujumiwa na jamii.
Hapo jana Papa Francis alifanya mazungumzo na rais wa wapalestina Mahmoud Abbas katika makao makuu ya Vatican.
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki alimtunuku Abbas medali ya Amani huku akimtaja kuwa ''malaika wa amani''
Watawa hao Marie Alphonsine Ghattas - aliyezaliwa katika familia ya kipalestina mjini Jerusalem alianzisha huduma ya watawa ya - Rosary Sisters, ambayo hadi wa leo inaendesha shule za chekechea na zile za msingi.
Bi Mariam anasemekana kuwa alitenda miujiza miongoni mwa jamii yake huku akitambuliwa kwa kuonekana na alama za ishara ya kusulubishwa kwa Yesu Kristo msalabani.
Wawili hao waliishi katika enzi ya Ottoman ambapo wanawake hawakuwa na semi katika hali halisi ya maisha lakini waliibuka kuwa mifano ya kuigwa licha ya kuishi maisha ya uchochole na magonjwa mengi.
No comments
Post a Comment