Wednesday, 6 May 2015

Rais Assad amshutumu Erdogan kuwa ndiye muuaji wa watu wa Syria

Rais Bashar Assad wa Syria amekosoa vikali siasa za serikali ya Uturuki kuhusu matukio ya sasa nchi hiyo na kumtaja Rais Recep Tayyip Erd... thumbnail 1 summary
Assad: Erdogan ni muuaji wa watu wa Syria
Rais Bashar Assad wa Syria amekosoa vikali siasa za serikali ya Uturuki kuhusu matukio ya sasa nchi hiyo na kumtaja Rais Recep Tayyip Erdogan wa Uturuki kuwa ni muuaji wa watu wa Syria.
Assad amesema Syria inapigana vita vikali na makundi kigaidi na wale wanaoyasaidia kwa fedha na silaha makundi hayo na kuongeza kuwa mtawala wa Kituruki wa utawala wa Kiothmania Ahmed Djemal Pasha alikuwa akiwanyonga Wasyria katika karne iliyopita na Rais Erdogan wa Uturuki ya sasa anaua na kumwaga damu za Wasyria katika kipindi hiki. Mtawala wa kijeshi Ahmed Djemal Pasha wa Uturuki aliamuru mauaji ya Waislamu wa madhehebu ya Shia na Wakristo wa Syria na Lebanon hapo mwaka 1916 katika miji ya Damascus na Beirut tarehe 6 Mei mwaka 1916.
Rais wa Syria amewataka wananchi wa nchi hiyo kuendelea kuliamini jeshi linalopambana na makundi ya kigaidi.
Makundi ya kigaidi kama lile la Daesh yanayoungwa mkono na kusaidiwa na nchi kama Saudi Arabia, Marekani, Qatar, Uturuki na utawala wa Kizayuni wa Israel yamekuwa yakifanya mauaji makubwa na ya kutisha katika nchi za Syria na Iraq kwa kipindi cha miaka minne sasa.

No comments

Post a Comment