Wednesday, 6 May 2015

Wapinzani Guinea wakubali kukutana na Rais Conde

Kiongozi wa kambi ya upinzani nchini Guinea Conakry amekubali wito wa kufan... thumbnail 1 summary

Kiongozi wa kambi ya upinzani nchini Guinea Conakry amekubali wito wa kufanya mazungumzo na Rais Alpha Conde wa nchi hiyo.
Msemaji wa kambi ya upinzani amesema uamuzi huo umechukuliwa kwa lengo la kutuliza ghasia ya machafuko ya wiki kadhaa sasa nchini humo.
Cellou Dalein Diallo anatarajiwa kukutana na Rais Conde Ijumaa ijayo ambapo pande hizo mbili zitajadili hali ya kisiasa na kijamii ya nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika.
Wafuasi wa kambi ya upinzani nchini Guinea Conakry wamekuwa wakifanya maandamano tangu katikati ya mwezi Aprili wakiitaka serikali kutazama upya tarehe ya kufanyika uchaguzi wa Rais. Watu wasiopungua watano wamekwishauawa katika ghasia na maandamano hayo.
  • Serikali ya Guinea imeainisha tarehe 11 Oktoba mwaka huu kwa ajili ya uchaguzi wa Rais na ule wa serikali za mitaa mwezi Machi mwaka 2016. Hata hivyo kambi ya upinzani inasema uamuzi huo unapingana na makubaliano ya mwaka 2013 ya kufanyika uchaguzi wa serikali ya mitaa kabla ya ule wa rais

No comments

Post a Comment