RAIS
Dkt. Jakaya Kikwete, ametamba kuwa angekuwa msanii wa muziki wa kizazi
kipya basi angelikuwa wa “BongoFleva” kutokana na kuwa na sauti nzuri
yenye kumudu kuimba nyimbo kwa ufasaha zaidi.
Kauli
hiyo ameitoa leo jijini Mwanza kwenye uwanja wa michezo wa CCM Kirumba
wakati wa maadhimisho ya kilele cha sherehe za Mei mosi zilizofanyika
Kitaifa jijini Mwanza kwa mwaka huu wa mwisho wa utawala wake.
Dkt.
Kikwete aliimba wimbo wa Bendi ya OSS (Ochestra Safari Sound) wenye
mashairi yasemayo "mimi msafiri bado niko njiani sijui lini nitafika...
naulizia watu kule ninakokwenda....” na kukonga nyoyo za mashabiki wa
muziki wa dansi waliomshangilia ambapo alijigamba kuwa na sauti ya
mauzo.
“Mmesikia sauti yangu si mbaya sana, hakika
nisingekuwa Rais wa Nchi hii basi nigekuwa msanii wa bongo fleva kama
akina Ali Kiba, Diamond na wasanii wengine wakali nikiuza album zangu
kwani ninge kuwa tishio kwa kuimba lakini sikujaliwa kuwa masanii lakini
najua kwa kiasi flani kuziimba nyimbo za baadhi ya bendi zilizokuwa
maarufu hapa nchini,” alisema.
Rais
pia alimpongeza msanii maarufu nchini wa kizazi kipya mwenye mashairi
na misamiati ya maneno magumu, Mrisho Mpoto, kwa kumtaka kujibu bango la
walimu lililokuwa na ujumbe uliosomeka “Shemeji Unatuachaje??” ambapo
alijibu kwa kusema kuwa kuoa mwalimu nitabu kweli kweli haya nimesikia.
Aliwapongeza
viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TUCTA) nchini kwa
kumwalika Mpoto “Mjomba” mara nyingi amekuwa akitoa ujumbe mzito kupitia
fani yake ya muziki na mashairi lakini yakifikisha ujumbe bara bara kwa
wananchi katika sherehe mbalimbali za kitaifa na makongamano .
No comments
Post a Comment