Friday, 15 May 2015

Rais KIKWETE aagiza baadhi ya majengo yabomolewe

Fri May 15 2015 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete maeneo yaliyoathiriwa v... thumbnail 1 summary
Fri May 15 2015
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akimuonesha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete maeneo yaliyoathiriwa vibaya na mafuriko huko Tegeta wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam
Rais JAKAYA KIKWETE ameuagiza uongozi wa wilaya ya KINONDONI jijini DSM kutumia PAMPU kuvuta maji yaliyotuama katika nyumba za watu na kubomoa majengo yaliyojengwa katika mikondo ama njia za asili za maji katika maeneo ya BASIAYA na NYAISHOZI TEGETA.

Akizungumza katika ziara ya kuyatembelea maeneo yaliyoathiriwa na mvua za masika Rais KIKWETE amerejea kauli yake ya kuwashauri wakazi waishio maeneo ya mabondeni kuyahama maeneo hayo na kuwa serikali ipo tayari kuwapatia viwanja vya kujenga nyumba katika maeneo yaliyo salama.

Rais KIKWETE amejionea mitaa iliyozama kabisa ndani ya maji katika eneo la BASIAYA na NYAISHOZI TEGETA katika wilaya ya KINONDONI na kuhoji hatua za dharura zilizochukuliwa na manispaa ya KINONDONI.

Eneo lingine ni katika kituo cha DAWASCO, TEGETA, ambapo Rais KIKWETE ameonyesha kushangazwa na ukimya wa wataalam wa maji waliozungukwa na maji katika eneo lao bila ya kuchukua hatua zozote.

Rais KIKWETE pia ametembelea eneo la KINONDONI MKWAJUNI ambapo amejionea nyumba zilizoathirika na maji katika eneo hilo na kusisitiza wakazi wa mabondeni kuyahama maeneo hao.

TBC

No comments

Post a Comment