Tuesday, 5 May 2015

Rwanda yatoa onyo kali Burundi

Nchi jirani ya Rwanda imeionya serikali ya Bunrundi na kuitaka iheshimu matakwa ya raia, ikieleza pia wasiwasi kuhusiana na ripoti kwam... thumbnail 1 summary

Nchi jirani ya Rwanda imeionya serikali ya Bunrundi na kuitaka iheshimu matakwa ya raia, ikieleza pia wasiwasi kuhusiana na ripoti kwamba waasi wa Kinyarwanda wanahusika katika vurugu hizo zinazopelekea maelfu ya wakimbizi kumiminika nchini Rwanda.
"Wakati tukiheshimu uhuru wa Burundi katika kushughulikia mambo yake ya ndani, Rwanda usalama wa raia wasio na hatia kama wajibu wa jumuiya ya kikanda na kimataifa," alisema waziri wa mambo ya kigeni Louise Mushikiwabo katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu.
"Rwanda inaitaka serikali ya Burundi kuchukuwa hatua zinazostahiki mara moja kuhakikisha inawalinda raia wake, kukomesha hali inayozidi kuwa mbaya ya kibinaadamu nam kurejesha amani," ilisema taarifa ya wizara ya mambo ya kigeni ya Rwanda.
Mushikiwabo alisema ana wasiwasi kuhusiana na ripoti kwamba vurugu nchini Burundi zinawahusisha waasi wa kabila la Wahutu walioko katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, maarufu kama Democratic Forces for the Liberation of Rwanda, FDLR.
Raia wa Burundi wakiwasili nchini Rwanda kufuatia vurugu zinazoendelea nchini mwao. Raia wa Burundi wakiwasili nchini Rwanda kufuatia vurugu zinazoendelea nchini mwao.
Waasi hao wamekuwa wakiendesha shguli zao mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika mikoa inayopakana na Rwanda na Burundi -- tangu walipovuka mpaka kutoka Rwanda baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ya watu hasa wa kabila la wachache la Watutsi.
Watu wasiopungua 24,000 wengi wao wakiwa wa kabila la Watusti wamekimbilia nchini Rwanda, wakihofia kuripuka kwa machafuko mengine ya kikabila, wamesema maafisa. Machafuko hayo yameitia wasiwasi hasa Rwanda, ambayo bado haijafuta kabisaa makovu ya mauaji ya mwaka 1994.

No comments

Post a Comment