Tuesday, May 19, 2015
Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar imesema kuwa wafanyabiashara wadogo wadogo hawatozwi kodi ya
vati (asilimia 18 ya mauzo)bali hutozwa asilimia 3 ya ushuru wa stempu.
Hayo yameelezwa na
Waziri wa Fedha Omar Yussuf Mzee leo katika ukumbi wa Baraza la
Wawakilishi Chukwani nje kidogo ya Mji wa Zanzibar wakati akijibu suala
la Mwakilishi wa Jimbo la Muyuni Jaku Hashimu Ayuob.
Alisema kuwa kiwango hicho cha asilimia tatu ( 3) kina lengo la kuwakuza na baadae kusajiliwa katika kodi ya vati.
Aidha Waziri Omar
Yussuf amesema kuwa Serikali haiwarudishi nyuma wafanya biashara
wadogowadogo bali ina nia ya kuwasaidia katika ukuwaji wa kibiashara
kwa lengo la kupata fursa ya kulipia kodi hiyo ya asilimia 3 kwa
vipindi vya miezi 3 ili kuwapa nafasi kushughulikia zaidi biashara zao.
Sambamba na hayo
amesema kuwa Serikali inazingatia mfumo mmoja wa ukusanyaji wa kodi
kutokana na kuwepo kwa taasisi nyingi zinasimamia kodi hizo hasa
ukizingatia kuwa kila taasisi zinakusanya kodi tofauti.
Wakati huo huo Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Muhammed Said Muhammed amesema kwamba
Serikali haina mpango wa kujenga kituo kipya cha huduma za mifugo katika
Jimbo la Muyuni kutokana na ukosefu wa kifedha.
Naibu Muhammed Said
amesema Wizara yake ina nia ya kuongeza vituo vipya vya mifugo Unguja
na Pemba pindi Serikali itakapowapatia kifedha.
Aidha amesema pamoja
na nia hiyo pia ina mpango wa kujenga nyumba za wafanyakazi katika
maeneo ya vituo hivyo ili wafugaji waweze kupata huduma kwa karibu
zaidi.
Naibu Waziri
amewapongeza wafugaji wote wa Unguja na Pemba kwa jitihada
wanazozichukuwa katika kujiendeleza kiufugaji kwani kufanya hivyo ni
kujitafutia ajira na kuweza kujitatulia matatizo madogomadogo.
ZANZINEWS.
No comments
Post a Comment