Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inatilia shaka nia ya serikali ya
Marekani inapotoa nara ya kupambana na kundi la kigaidi la Daesh (ISIS).
Hayo yamesemwa na Waziri wa Ulinzi wa Iran Brigedia Jenerali Hussein
Deqhan alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Fouad Maasoum wa Iraq
mjini Baghdad. Dehqan ameongeza kuwa Marekani inaibua migogoro na kuunga
mkono makundi ya kigaidi kupitia nchi waitifaki wake katika eneo na kwa
njia hiyo Washington inatekeleza stratijia ya kuvuruga usalama wa nchi
zenye misimamo huru na zinazojitegemea. Amesema awali Marekani
ilisitasita katika kutoa msaada kwa watu wa Iraq katika vita dhidi ya
Daesh na hilo linaonesha wanafuatilia malengo ya nyuma ya pazia katika
kile wanachodai ni vita dhidi ya kundi hilo la kigaidi. Brigedia
Jenerali Deqhan amesema Iran daima imekuwa ikiwaunga mkono watu wa Iraq
pasina kuzingatia masuala ya kikaumu n.k. Kwa upande wake Rais Fouad
Maasoum wa Iraq ameashiria uhusiano mzuri wa Iran na Iraq katika nyanja
zote na kusema nchi yake ingali inahitajia msaada na himaya ya Iran
katika sekta zote. Amesema kundi la kigaidi la Daesh linalenga kuibua
hitilafu za kikaumu na kimadhehebu na kuongeza kuwa magaidi hao
wanafuatia ile ile itikadi ya utawala wa Baath uliopinduliwa Iraq.
Maasoum amesema magaidi wa Daesh hawatafuatishi baina ya Sunni na Shia
wala baina Wakurdi na Waarabu au Waislamu na Wakristo na kwamba wote hao
ni waathirika wa jinai za Daesh. Amesema leo Iraq inahitaji umoja wa
kitaifa ili kupemabana na magaidi wanaotaka kuisambaratisha nchi hiyo.
Tuesday, 19 May 2015
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments
Post a Comment