Thursday, 7 May 2015

Simba yaiendea kambini JKT Ruvu

Simba yaiendea kambini JKT Ruvu           WEKUNDU wa Msimbazi Simba wameingia kambini jana kwa ajili ya kujiandaa na... thumbnail 1 summary
Simba yaiendea kambini JKT Ruvu
     






   
 
 
WEKUNDU wa Msimbazi Simba wameingia kambini jana kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wao wa kumaliza msimu dhidi ya JKT Ruvu utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa, Dar es Salaam keshokutwa.
Simba yenye pointi 44 endapo itashinda mchezo huo uliobaki, itamaliza ligi ikiwa na pointi 47.
Akizungumza na gazeti hili jana msemaji wa Simba Haji Manara alisema kikosi kinatarajia kumaliza kwa ushindi mnono ili baada ya hapo kijipange kwa ajili ya msimu mpya.
“Tunataka tumalize ligi kwa ushindi, tunawafahamu JKT Ruvu sio timu ya kubeza, kwa sasa hatuna cha kugombea lakini inapendeza tukamaliza kwa ushindi wa nguvu,”alisema.
Alisema wachezaji wote wako vizuri na wanategemewa kuongoza kikosi hicho vyema katika mchezo huo wa mwisho.
Manara alisema baada ya mchezo huo wa mwisho wanakusudia kujipanga upya ili kuanza msimu mpya wakiwa na lengo la kufanya vizuri zaidi.
Tangu kuanza kwa msimu huu Simba ilikuwa ikisua sua hali ambayo ilizua wasiwasi wa kushuka daraja lakini walifanya mabadiliko makubwa na kufanikiwa kuwa katika nafasi tatu za juu.
Simba tayari wamecheza michezo 25, wameshinda 12, sare nane na kupoteza michezo mitano.

No comments

Post a Comment