Monday, 18 May 2015

Takukuru kusambaza makachero majimboni

Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hosea TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inatarajia kusambaza vijana wa kazi katika ... thumbnail 1 summary
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward HoseaMkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward HoseaTAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) inatarajia kusambaza vijana wa kazi katika majimbo yote nchini, kuwashughulikia wote walioonesha nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uchaguzi, ambao wanatoa rushwa ili kupata wafuasi.
Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru, Dk Edward Hosea, alisema hayo jana alipokuwa akijibu agizo alilopewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika katika semina ya wabunge wa Mtandao wa Wabunge wa Afrika wa Kupambana na Rushwa (APNAC), tawi la Tanzania.
Mkuchika alimtaka Dk Hosea asisubiri kipenga cha kampeni kuanza, bali asambaze vijana wake kwenye majimbo ya uchaguzi kwani viashiria vya rushwa vimeshaanza.
“Kazi imeanza, waambie vijana wako wasisubiri Oktoba, waanze kazi sasa maana kuna viashiria vya rushwa, waingie wafanye kazi,” alisema Mkuchika.
Alisema semina hiyo imekuja wakati mzuri wanapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu, hivyo ni vyema wabunge wakumbuke wana wajibu wa kulinda maadili na kuepuka vitendo vya rushwa.

No comments

Post a Comment