Sunday, 3 May 2015
Tunisia yasema iko tayari kuwalinda mahujaji wa kiyahudi
Tunisia imesema leo jumapili kwamba hatua za kiusalama zimechukuliwa ili
kuwalinda mahujaji wa kiyahudi katika tamasha la kidini linalotarajiwa
kufanyika baadaye wiki ijayo katika kisiwacha Djerba. Tunisia imetoa
tamko hili baada ya Israel kutoa tahadhari juu ya kitisho cha shambulizi
la kigaidi katika tamasha hilo. Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu amesema
hapo jana kwamba nchi yake imegundua vitisho vya mashambulio ya ugaidi
dhidi ya mayahudi au maeneo ya waisraeli katika nchi hiyo ya Kaskazini
mwa Afrika. Hata hivyo serikali ya Tunisia ilikanusha mara moja taarifa
hiyo. Waziri wa mambo ya ndani wa Tunisia Najem Gharsalli amewaambia
waandishi habari akiwa Djerba, kisiwa kunakofanyika tamasha hilo la kila
mwaka, kwamba maafisa wa usalama na jeshi wako tayari kuimarisha
usalama wakati wa tamasha hilo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments
Post a Comment