Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema mamia ya wanawake na watoto waliojaa hofu, waliookolewa kutoka kwa wanamgambo wa Boko Haram, wamepelek...
13:01
Msemaji wa jeshi la Nigeria amesema mamia ya wanawake na watoto waliojaa
hofu, waliookolewa kutoka kwa wanamgambo wa Boko Haram, wamepelekwa
katika kambi moja ya wakimbizi Mashariki mwa mji wa Yola. Wanawake na
watoto 275 ambao wengine walionekana kuwa na majeraha mikononi na
vichwani waliwasili katika kambi hiyo inayoendeshwa na taasisi ya
kitaifa inayosimamia usaidizi wa dharura siku ya jumamosi usiku, baada
ya kusafiri kwa muda mrefu barabarani. Mwanamke mmoja aliyepata jeraha
katika mguu wake baada ya kupigwa risasi, amesema walikuwa wameketi
chini ya mti wakati jeshi lilipowasili na kuanza kupambana kwa
kufyatuliana risasi na wanamgambo hao, jambo lililopelekea wengi wao
kupata majeraha ya risasi. Bado haijawa wazi ni watu wangapi waliotekwa
nyara na Boko Haram lakini shirika la Amnesty International linakadiria
wanamgambo hao wanaotaka Mataifa ya Afrika Magharibi kuwa chini ya
sheria ya itikadi kali, wamewateka nyara zaidi ya wanawake na wasichana
2000 tangu mwanzo wa mwaka 2014.
No comments
Post a Comment