Wednesday, 6 May 2015

Uchaguzi Uingereza waitia kiwewe EU

Uchaguzi mkuu wa Uingereza unakuja na hatari kubwa, si tu kwa siasa za ndani ya Uingereza, lakini pia bara la Ulaya kwa ujumla: Baadhi wanah... thumbnail 1 summary
Uchaguzi mkuu wa Uingereza unakuja na hatari kubwa, si tu kwa siasa za ndani ya Uingereza, lakini pia bara la Ulaya kwa ujumla: Baadhi wanahofu kuwa kura hiyo inaweza kuwa mwanzo wa Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya.
Wakati wapigakura watakapoelekea vituoni Alhamisi wiki hii (Mei 8), wanasiasa wa nchi hiyo hawatakuwa pekee watakaosubiria matokeo ya mwisho kwa wasiwasi. Hali ya mashaka itatawala barani Ulaya kote pia, kukiwa na wasiwasi kwamba kile kinachojulikana kama "Brexit" kinakaribia.
Neno hilo lililotungwa kuelezea uwezekano wa Uingereza kujiondoa kwenye Umoja wa Ulaya - limekuwa likisikika mara kwa mara mjini Brussels, yaliko makao makuu ya umoja huo, tangu waziri mkuu wa Uingereza David Cameron alipoahidi kuitisha kura ya maoni juu ya uanachama wa Umoja wa Ulaya, ikiwa chama chake kitashinda uchaguzi mkuu wa mwezi huu.
Michael Emerson, kutoka kituo cha ushauri juu ya masuala yanayohusiana sera ya Ulaya, alisema uundwaji wa serikali ijayo unaweza kuwa tu mwanzo wa mashaka. " Kuondoka kwa Uingereza kunaweza kusababisha uharibifu usiyoelezeka kwa ukamilifu na uaminifu wa Umoja wa Ulaya, aliongeza mchambuzi wa kituo cha Carnage Europe Jude Dempsey, na kusema kuwa Cameron ameiweka Uingereza kwenye njia ya msuguano na washirika wake wa Ulaya, jambo alilolitaja kuwa hatari.
Wagombea wa upinzani wakiwa katika mjadala wa televisheni. Wagombea wa upinzani wakiwa katika mjadala wa televisheni.
Kiini cha mizozo na malumbano
Lakini Cameron hajawahi kuona haya kuutikisa Umoja wa Ulaya. Katika miaka michache iliyopita, amekuwa kiini cha wasiwasi na malumbano kuhusu kila kitu, kuanzia bajeti za jumuiya hiyo, hadi kwenye nfasi za juu za ajira, uhamiaji na sheria mpya kuhusu nidhamu ya fedha. Uchunguzi wa maoni unaonyesha kuwa Waingereza ni watu wasioupenda Umoja wa Ulaya, licha ya kuwa wanachama wa jumuiya hiyo kwa zaidi ya miaka 40.. source DW. may 6, 2015

No comments

Post a Comment